Jaribu ujuzi wako. Soma kila sentensi, amua kama ni kweli au si kweli, kisha angalia jibu.
Maswali 10
- Watu wenye kisukari hawapaswi kula ugali kabisa. Si kweli. Unaweza kula ugali kwa kiasi, hasa wa dona, pamoja na mboga na protini.
- HbA1c inaonyesha wastani wa sukari kwa miezi 2 hadi 3. Kweli.
- Ukijisikia vizuri, unaweza kuacha dawa. Si kweli. Kisukari mara nyingi hakina dalili. Acha au badilisha dawa kwa ushauri wa daktari tu.
- Kutembea baada ya kula husaidia kushusha sukari. Kweli.
- Kisukari cha aina ya 2 hutokea kwa watu wenye uzito mkubwa tu. Si kweli. Hata watu wembamba wanaweza kupata kisukari.
- Sukari chini ya 4 mmol/L ni hatari na inahitaji hatua ya haraka. Kweli.
- Asali haipandishi sukari kama sukari ya kawaida. Si kweli. Asali nayo hupandisha sukari ya damu.
- Kuangalia miguu kila siku kunaweza kuzuia kukatwa mguu. Kweli.
- Insulini husababisha upofu. Si kweli. Sukari iliyo juu kwa muda mrefu ndiyo huharibu macho, si insulini.
- Kisukari kinaweza kudhibitiwa na mtu akaishi maisha marefu yenye afya. Kweli.
💡
Umepata mangapi?
Kama ulikosa zaidi ya mawili, soma makala zetu za Matokeo na Lishe, au muulize Tulia swali lolote kwenye WhatsApp.



